Job 20:19-23

19 aKwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu;
amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga.

20 b“Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana;
hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.
21 cHakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale;
kufanikiwa kwake hakutadumu.
22 dKatikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata;
taabu itamjia kwa nguvu zote.
23 eAtakapokuwa amelijaza tumbo lake,
Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake,
na kumnyeshea mapigo juu yake.
Copyright information for SwhNEN